Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Messi ametaja goli lake bora muda wote kati ya magoli yake 552

on

Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina anayeichezea club ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi amelitaja goli lake bora alilowahi kulifunga kati ya magoli yake 552 aliyowahi kuyafunga katika maisha yake ya soka.

Messi hadi sasa amecheza jumla ya game 637  katika mashindano yote na amefunga jumla ya magoli 552, ila ukimuuliza goli lake bora alilowahi kufunga anasema yeye goli lake bora halipimi kwa uzuri ila umuhimu wake.

Lionel Messi amelitaja goli lake la kichwa alilolifunga katika mchezo wa fainali ya UEFA Champions League kati ya FC Barcelona dhidi ya ManUnited mjini Roma Italia ndio goli lake bora katika magoli yake yote aliyowahi kuyafunga.

FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018

Soma na hizi

Tupia Comments