Top Stories

Ombi la Mbunge wa Same Dr Mathayo kwa Wananchi wake kuhusu Rais Magufuli

on

Mbunge wa jimbo la Same Magharibi  CCM Dr Mathayo David Mathayo amewaomba wananchi wa  Jimbo la Same Magharibi kumuunga mkono na kumuombea afya njema Rais Dr John Magufuli ili aweze kuendelea kuiongoza Tanzania izidi kupata maendeleo na kurudisha nidhamu katika sekta mbalimbali nchini.

Dr Mathayo ametoa kauli hiyo katika siku ya kwanza ya ziara yake ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kama aliyoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa jimbo hilo ambapo akizungumza na wananchi wa kata za Msindo, Mshewa na Mhezi mhemiwa Mathayo amesema serikali ya awamu ya tano imeonesha mafanikio lukuki katika Nyanja mbalimbali.

Mbunge huyo amekabidhi vifaa mbalimbali alivyoahidi katika kata hizo zikiwemo pia fedha taslimu huku akitoa rai kwa uongozi wa kila kata kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Katika kata ya msindo Dr Mathayo ametoa fedha ,mifuko ya saruji,mabomba ya maji,ambapo katika kata ya mshiwa Dr Mathayo amekabidhi mifuko ya saruji na fedha taslim kwa ajili ya shughuli za marendeleo kiasi cha Tsh milioni 13 laki 9 na Zaidi ya shilingi milioni tisa katika kata ya Mhezi Zaidi ya shilingi milioni tisa na mifuko ya saruji.

VIDEO: Wanafunzi wa masomo ya fizikia kwenye uthubutu wa kutatua matatizo ya kiteknolojia

Soma na hizi

Tupia Comments