AyoTV

Haji Manara hakaukiwi kila siku mpya “Iga Ufe Thisi Is Next Level”

on

Kuelekea Simba wiki uongozi wa club ya Simba SC ilifanya mkutano na waandishi wa habari leo jiji Dar es Salaam na kuzungumzia maandalizi yao ya wiki ya Simba SC na kilele cha SImba Day, kuelekea tamasha hilo afisa habari wa Simba SC Haji Manara alizindua slogan yao mpya itakayotumika katika maadhimisho ya wiki ya Simba.

Haji Manara ametangaza rasmi kwa ukubwa wa tamasha lao la Simba Day linaloelekea miaka 10 sasa toka kuanzishwa kwake, wametangaza kuwa kauli mbiu au slogan yao kwa mwaka 2019 ni “Iga Ufe This Is Next Level”

“Huu ni mwaka wa 10 mfululizo toka enzi za akina mzee dalali hatukatazi watu kuiga Kenya wameiga Uganda wameiga Ghana wameiga, jambo jema linaigwa tu ni jambo jema kuiga hasa unaiga jambo lililokuwa zuri, katika kuiga sasa lazima tunawasaidie wanaotuiga ili waifanye katika ubora, kauli mbiu yetu ya Simba Wiki IGA UFE THIS IS NEXT LEVEL”>>>Haji Manara

VIDEO: Kauli ya Kaseja baada ya kuichezea Taifa Stars baada ya miaka 6

Soma na hizi

Tupia Comments