Kwa zaidi ya wiki moja sasa huduma ya mtandao ya WhatsApp imefungwa na serikali ya China ikielezwa kuwa ni kwaajili ya kuimarisha usalama kabla ya kufanyika kwa mkutano wa chama cha Kikomunisti mwezi ujao.
Imeelezwa kuwa wakati mwingine, mawasiliano hayo ya WhatsApp yamekuwa yanapatikana kupitia mtandao binafsi wa VPN ambao unasimamia mitandao ya China pekee.
Pia imeelezwa kuwa mwezi Julai viliwekwa vikwazo vya watumiaji wa mtandao huo kutuma picha hata video kwa watu wengine wa China. WhatsApp inaripotiwa kuwa huduma pekee ya mtandao iliyokubalika na serikali hiyo kuwa nchini humo.
Ulipitwa na hii? WATANZANIA: Kuongea na simu kwa zaidi ya dakika 6 ni HATARI