Moja kati ya vitu ambavyo wajawazito hawaruhusiwi kabisa kuvifanya ni pamoja na kunywa pombe ya aina yoyote ile ingawa hata hivyo wapo baadhi ya wanawake huamini mvinyo ‘wine’ huwa haina madhara kwa ujauzito hasa kama mjamzito atainywa kwa kiwango kidogo sana.
Katika utafiti mpya uliofanywa Marekani siku za karibuni umeonesha kuna madhara makubwa kwa watoto wanaozaliwa endapo mama zao walijihusisha na pombe ya aina yoyote na kiwango chochote hivyo wameshauri wanawake wasitumie kabisa vileo vyovyote wakiwa na ujauzito.
Miongoni mwa athari zilizotajwa na watafiti hao ambazo husababishwa na ulevi wakati wa ujauzito ni pamoja na mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake au ujauzito kuharibika, mtoto kuzaliwa na uzito mdogo, mtoto kuzaliwa na matatizo ya moyo, ini au mifupa.
Pia mtoto kuwa mzito katika kujifunza, matatizo ya kuona na kusikia, kichwa kikubwa au kuwa na uso wenye matatizo na mengineyo.
ULIPITWA? Mikoa mitano imetajwa kuwa hatarini kuingiliwa na Wanyamapori
Hii je? RC MWANZA! Kaacha ofisi kuwafuata Wananchi, unamweleza changamoto zako