Top Stories

Waziri Kigwangalla ameteua wajumbe hawa wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro

on

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangalla leo January 19, 2108 ameteua Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro yenye wajumbe 12. Hii ni baada ya Rais John Magufuli kumteua Prof. Abiud Lucas Kaswamila kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo December 1, 2017.

Wajumbe hao ni pamoja na Brigedia Jenerali (Mstaafu) Aloyce Damian Mwanjile, Bakari Nampenya, Dk. Deogratius Michael Pisa, Edward Ndulet, Freddy Manongi, Haruna Masebu na Humphrey Hilary Muniachi.

Wengine ni Jumanne Feruzi, Prof. Kalunde Pili Sibuga, Michael Kamazima, Mhandisi Peter Rudolf Ulanga, na Ruzika Muheto.

“Tumekuja kwa heshima, ukidharau timu inakufanyia mambo” Kocha Simba

“Nimekaa ndani wiki 3, nimeona waliosema nina VVU” – STEVE NYERERE

Soma na hizi

Tupia Comments