Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwamo kusambaza dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi ‘ ARV’s ‘ na kusababisha hasara ya Sh.Mil 148.
Madabida na wenzake wamefunguliwa kesi hiyo mpya namba 80 ya 2017, baada ya mahakama leo kuwafutia kesi kama hiyo iliyofunguliwa mwaka 2014, ambapo baada ya kesi hiyo kufutwa, Madabida ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho na wenzake walikamatwa tena na kufunguliwa kesi mpya ya uhujumu uchumi.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hao hawakurusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka hadi Mahakama Kuu. Wakili wa Serikali, Pius Hilla alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika lakini DPP bado hajafanya maamuzi kama kesi hiyo isikilizwe Kisutu ama Mahakama Kuu.
Kutokana na hoja hiyo Wakili Hilla aliomba wapewe muda, ambapo mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi December 7, 2017 (kesho) ili upande wa mashtaka ujibu hoja.
Ulipitwa na hii? Waliosababishia hasara ya Sh.milioni 370 kwa TCRA wafikishwa Mahakamani