Waziri wa Viwanda na Biashara Suleiman Jafo leo amezindua zoezi la ulipaji wa fidia katika mradi wa magadi soda ambapo Serikali, baada ya miaka mingi, imefika Monduli leo na kulipa fidia ya Tsh bilioni 14.48. Kati ya hizo, bilioni 6.2 zinakwenda moja kwa moja kwa wananchi 499.”
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ulipaji wa fidia kwa mradi wa magadi soda Engaruka leo Jijini Arusha, Januari 23, 2025, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fredrick Edward Lowassa, amesema kuwa mradi huo umekuwa ukisuasua kwa zaidi ya miaka 20.
Lowassa amesema tayari wanamazingira wametoa cheti kinachothibitisha kwamba mradi huo hauharibu mazingira.
Magadi ni kemikali inayotumika viwandani kuzalisha vioo, sabuni, rangi, karatasi, kusafishia mafuta ya petroli, kusafishia madini, kutengenezea mbolea na kusafishia maji.
Kwa kuvuna magadi hayo, Tanzania itakuwa imeanzisha kiwanda mama na kujiweka katika nafasi nzuri ya kukuza na kuibua kwa kasi viwanda vinavyotumia magadi kama malighafi katika uzalishaji.
Kwa mujibu wa tafiti, magadi yatakayozalishwa yataweza kutosheleza mahitaji ya magadi hapa nchini na mengine kuuzwa nchi za nje.