AyoTV

VIDEO: Majibu ya Rais wa TFF kuhusu tuhuma za kula bilioni 1 kutoka FIFA

on

Baada ya headlines za muda mrefu kuhusu tuhuma za Rais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi kudaiwa kutumia kinyume na taratibu kiasi cha zaidi ya Tsh bilioni moja ya TFF iliyotolewa na shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA.

Leo February 7 2017 Malinzi ameweka wazi kuhusiana na tuhuma hizo na kudai kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi, hivyo amezisikia hizo tuhuma na kuwaomba wanaodai hivyo waombe au waangalie taarifa za account za bank za TFF kuhusiana na madai hayo.

“Unajua uendeshaji wa mpira ni mgumu sana na naomba msisahu kuwa tunaingia kwenye uchaguzi mwaka huu mwezi wa kumi, lakini kama kuna watu ambao watapenda kugombea nafasi za TFF watulie muda ukifika wa kuchukua fomu na kugombea utafika”

Hilo mliloniuliza nimelisikia sio kwamba sijasikia na hizo hesabu zilizosemwa nimezisikia na yanayoendelea nayajua, hata hicho kiasi cha 1.5 wanachokisema ni dola 550,000 ambazo ni pesa kutoka FIFA, ndio maana nimewakumbushia kuwa kuna pesa tunaisubiria kutoka FIFA toka mwaka jana haijafika kwa sababu utaratibu umebadilika sasa hivi

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments