Shirikisho la soka Ulimwenguni (FIFA) linadaiwa kuwa limekataa ombi la Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutaka kabla ya mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Ufaransa siku ya Jumapili kuchezwa, ichezwe video yake uwanjani hapo ili kuhamasisha amani.
Zelensky inadaiwa kuwa aliomba hilo huku akitaka kuonekana katika video hiyo akitoa ujumbe wa kuhamasisha amani wakati huu Ukraine ikiwa katika vita kutokana na kuvamiwa na Urusi.
Taarifa za ndani kutoka mailSports zinaeleza kuwa FIFA wamemkatalia Zelenaky ombi hilo pasipo kumpa sababu za kukataa.
Rais Volodymyr Zelensky amekuwa akihutubia kwa njia mbalimbali katika matukio makubwa Duniani kuhusu amani ikiwa inatafsiriwa kama ishara kuomba sapoti katika vita dhidi ya Urusi.