Shirikisho la soka duniani limekashifiwa kwa kutochukua hatua juu ya kuendelea kwa ukatili wa Israel huko Palestina, huku wataalam wakitoa wito kwa FIFA kwa viwango vyake viwili, ripoti ya Al Jazeera.
Kufuatia mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine, FIFA iliharakisha kuifungia timu ya Urusi kutoka kwa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022 huku baraza la Ulaya likizitimua vilabu vya Urusi kutoka kwa mashindano yake yote.
Hata hivyo, FIFA na UEFA bado hawajachukua hatua dhidi ya Israel licha ya mashambulizi yake kusababisha mauaji ya Wapalestina zaidi ya 13,000 huko Gaza tangu Oktoba 7.
“Kuna wachezaji, timu na familia ambazo zinateseka kutokana na kile kinachotokea [nchini Palestina].
FIFA haijasema lolote,” Simon Chadwick, profesa wa michezo na uchumi wa kijiografia katika Shule ya Biashara ya Skema, aliiambia Al Jazeera.