Michezo

FIFA yapanga kuvinusuru vyama vya soka vilivyoyumba kiuchumi kisa corona

on

Baada ya mlipuko wa virusi vya corona kutokea na kutangazwa kama janga la kidunia, mambo mengi na taasisi nyingi za soka zimeyumba kiuchumi kutokana kusimama kwa Ligi.

Shirikisho la mchezo wa soka Ulimwenguni FIFA linapanga kuandaa mpango maalum wa kuzipatia pesa taasisi za soka ambazo zimeyumba kiuchumi.

FIFA inao mfuko wa akiba wa pesa kwa ajili ya mambo ya dharula ila kutokana na janga hili, sasa imekiri wazi ni wakati sahihi kutumika kwa ajili ya kunusuru taasisi hizo.

Soma na hizi

Tupia Comments