Michezo

Kama uliikosa ya muonekano wa Mbwana Samatta, Lionel Messi na Neymar kwenye Game ya FIFA 16

on

Kwa wapenzi wa michezo ya game hususani game za mchezo wa soka maarufu kama Play Station, huwa ni kawaida kuona wataalam wa game kutengeneza game za timu zinazopendwa na muonekano wa wachezaji wa timu husika lengo likiwa kujenga taswira halisi kwa mchezaji wa game.

fifa-17-no-messi

Huu ndio muonekano wa Lionel Messi katika Game ya FIFA 16

Kama uliikosa Mbwana Samatta ambaye amejiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kongo kwa dau linalotajwa kuwa ni euro 800,000, ameingizwa katika ya Play Station ya FIFA 16.

Screenshot_2016-03-02-16-10-53-1

Huu ndio muonekano wa Mbwana Samatta ambapo kwa taarifa zisizo rasmi anatajwa kuwa huenda akawa mtanzania wa kwanza kuwemo katika Game ya FIFA 16

Samatta yupo katika game hiyo na nimekutana na muonekano wake sambamba na namba yake ya jezi 77 anayotumia, kwa ripoti zisizo rasmi huenda Mbwana Samatta ndio akawa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kuwemo katika hiyo.

fifa-16-release-date

Muonekano wa wachezaji wa FC Barcelona akiwemo Neymar wa kwanza kulia katika Game ya FIFA 16

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments