Ni agizo jipya kutoka shirikisho la soka duniani FIFA ambalo limetumwa nchini Tanzania liifikie Club ya soka ya Yanga na litekelezwe ndani ya wiki moja.
Mwenye mamlaka ya kuzitoa habari zote za TFF Afisa habari Alfred Lucas ameiambia AyoTV yafuatayo >>> ‘FIFA imetuandikia barua ikitaka tuisimamie Yanga maswala mbalimbali lakini kubwa ni madai ya kocha wa zamani wa Yanga anayadai, Mholanzi Ernest Brandit walivunja mkataba na Yanga‘
‘Alishapeleka madai yake kwenye kamati ya hadhi ya Wachezaji FIFA ikatoa uamuzi June 2015 wa kumlipa kocha huyo USD 11000 ambayo inafikia Tsh. 24.5 Milioni na utekelezaji wa maamuzi yale Yanga haijayafanya hadi leo‘
‘FIFA wametuma waraka wakiitaka Yanga ifanye hilo jambo kabla ya kuingia kwenye kamati ya nidhamu sababu wakiingia kwenye kamati ya nidhamu watakabiliwa na adhabu, faini zaidi ya hiyo au kuporwa pointi za ligi kuu ilizovuna‘
Unaweza kutazama video ya kauli ya TFF kwenye hii video hapa chini