Uongozi wa FIFA unakutana leo makao makuu ya shirikisho hilo Zurich Uswiss ili kupanga tarehe ya uchaguzi wa rais atakaye mrithi Sepp Blatter.
Blatter na viongozi wengine wa Kamati ya utendaji ya FIFA watakuwa na mkutano wa kupanga ratiba ya kumchagua Rais ajaye.
Hata hivyo miongoni mwa ajenda za mkutano huo ni kupanga jinsi ya kukabiliana na rushwa ambazo tayari ziliikumba FIFA na huenda wakaweka muda wa Rais kuwa madarakani… Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Blatter kufanya mkutano toka alipotangaza kujiuzulu June 2 2015.
Blatter alitangaza kujiuzulu kutokansa na viongozi saba wa FIFA akiwemo Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Jeffrey Webb kutuhumiwa kwa rushwa na kutakatisha fedha haramu… Hata hivyo kwa mujibu wa Sheria za FIFA mgombea anapaswa atangaze nia miezi minne kabla ya tarehe ya uchaguzi.
Wanaotajwa kugombea nafasi ya Urais wa FIFA hadi sasa ni Jordan Prince Ali bin Al Hussein ambaye aligombea mwezi May na kushindwa na Blatter na mwingine ni rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) Michel Platini licha ya wao kutoweka bayana.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.