Tumekuwa tukisikia mitaani stori mbalimbali kuhusu filamu zilizofungiwa huku tukiwa hatuna uhakika na kile tukisemacho lakini millardayo.com imepata nafasi ya kufanya exclusive interview na Joyce Fisoo ambae ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania.
Anasema>>>’Nadhani hupaswi kujua filamu zilizofungiwa bila kujua filamu ngapi zimewasilishwa, toka mwaka 2011 mpaka sasa tumepokea na kushughulikia filamu zipatazo 1059 ikiwa ni kwa maana ya majina lakini ukizungumzia sehemu ya kwanza na ya pili ( Part I & II ) ni jumla ya cd 2118 kuanzia mwaka 2011 mpaka january 2014′
‘Kuanzia July 2013 mpaka January 2014 tumepokea filamu 570 napenda kukufahamisha katika filamu 570 hakuna filamu iliyozuiwa kwenda kwenye jamii, kati ya filamu 1059 tumeweza kuelekeza kufanyiwa marekebisho filamu 123 kutokana na kutokua na maneno au maadili sahihi ya kuonyeshwa kwa jamii ambapo filamu hizo ni sawa na asilimia 5.8 ya filamu zote zilizowasilishwa kwenye bodi’
‘Kati ya mwaka 2011 mpaka 2013 jumla ya filamu 7 zilizuiliwa ambazo ni sawa na asilimia 0.33, Filamu hizo tulizozuia kati ya mwaka 2011 mpaka 2013 ni pamoja na Inye, Inye Plus, Inye Ngwede Ngwede, Inye Ndembe ndembe,Mtoto wa Mama,Tifu la Mwaka na Sister Mary’
‘Mwaka 2013 July mpaka 2014 January hakuna filamu tulizozuia lakini zipo filamu 16 zilizoelekezwa kufanyiwa marekebisho, filamu 14 zimesharudishwa kwetu tumeridhia na tumeshazipa kibali lakini filamu mbili bado maeneo tuliyoekeza kufanyiwa marekebisho hazijarejeshwa ambazo ni Mv Spice ya mwigizaji Frank na Filamu ya Nimekubali Kuolewa ya Dr. Cheni, naomba ieleweke kwamba hakuna filamu iliyozuiwa kwa mwaka wa 2013 July mpaka January 2014.
Huu hapa chini ni mfano wa filamu iliyokaguliwa na kupewa daraja.