AyoTV

Wema kaongea kuhusu Diamond kumpost Instagram

on

July 5, 2016 mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz aliingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kupost kwenye Instagram kuhusu watu kujitokeza kwa wingi kwenye show ambayo imeandaliwa na mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu pamoja na Christian Bella na Idris.

AyoTV ilimpata Wema na ameyasema haya >>>Watu wamekuwa wakiitumia hii beef yetu kujipatia followers hasa kwenye mitandao yao kwasababu mtu anaweza akatokea sehemu yoyote na kuanza kunitukana mimi au kumtukana Naseeb akajipatia followers wa kutosha, kuna muda mimi nilikuwa naogopa kuimba wimbo wa Diamond unapopigwa naogopa hata kucheza’

Nikisikia nyimbo za Naseeb siwezi kuimba inanibidi nikaze lakini mwisho wa siku najikomoa mimi mwenyewe nikikaa kwenye gari nitaimba kama utakuwa unakumbuka nilivyoimba mara ya kwanza watu wakashangaa wakawa wanajiuliza maswali mengi sana, kwasasa hatuko kwenye mapenzi lakini tunasaidiana kazi kuonesha uzalendo’

ULIIKOSA HII COMMENT YA SHABIKI AMBAYO WEMA HATOISAHAU BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments