Mix

Msikiti mwingine uliyotajwa kuungua moto Dar es salaam Sept 18.

on

Capture3Kwa matukio ya kuungua moto kwa msikiti kwa kipindi cha miezi miwili hii imekua ikifululiza sana ambapo August 13 msikiti wa Mtambani ambao uko maeneo ya Kinondoni Manyanya uliungua upande wa juu.

September 12 msikiti huo huo wa Mtambani uliungua tena na sababu iliyotajwa ni kama ya mwanzo kuwa ilitokea hitilafu ya umeme,taarifa nyingine iliyonifikia ni kuungua kwa msikiti mwingine leo Dar es salaam.

Huu ni Msikiti wa madhehebu ya Wahindu ambao upo Mtaa wa Kibasila leo umeteketea kwa moto na baadhi ya mali kusemekana zimeungua na mtu mmoja kukimbizwa hospitali kutokana na mshituko.

Miongoni mwa mashuhuda wa tukio hili amesema kuwa moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye mashine ya luku.

Capture4

Capture2

Capture1

Picha:Global Publishers.

Tupia Comments