Top Stories

DRC: Waandishi waitisha mgomo usio na kikomo baada ya mwandishi mwenzao kutekwa

on

Leo January 12, 2018 taarifa ambazo zimeshika headlines kutokea nchini DRC Congo ni kuhusu waandishi wa habari nchini humo wameitisha mgomo usio na kikomo baada ya kutekwa kwa mwandishi mwenzao.

Mwandishi wa habari wa Radio China (CRI), Molelwa Mseke Jide ameiambia Ayo TV na millardayo.com kuwa waandishi wa Habari wa mji wa Beni nchini humo walikuwa kwenye kikao cha kuazimia mgomo huo.

Jide amesema kuwa mwandishi aliyetekwa ni Kiongozi Mkuu wa Radio Graben iliyopo mji wa Goma anayeitwa Kasereka Jadomwangwingwi.

Ameeleza kuwa mwandishi huyo alitekwa jana January 11, 2018 saa 11 jioni akiwa ndani ya msafara wa magari yaliyokuwa yakitokea mji wa Kasindi ambao upo mpakani mwa Congo na Uganda akielekea mji wa Beni.

Akisimulia mkasa huo Jide amesema msafara wa mwandishi huyo na watu wengine ulitekwa na majambazi waliovalia sare zilizofanana na za jeshi la taifa, ambapo waliwachukua watu wengine akiwemo na yeye.

‘Lowassa akiamua kurudi CCM hatuogopi, Ila sidhani’ Makamu Mwenyekiti

RC Makonda azungumzia ujio Rais wa Rwanda Paul Kagame

 
 

Soma na hizi

Tupia Comments