Top Stories

President JPM amewapongeza JKT na Magereza baada ya kutimiza haya

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo February 3, 2018 amewatunuku kamisheni maafisa wanafunzi 197 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  kundi la 62/17 katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kati ya maafisa hao, 188 wamepata mafunzo ya kijeshi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha (TMA) yaliyoanza January 23, 2017 na 9 wamepata mafunzo katika nchi za Burundi, Kenya, China na Uingereza, na wote wametunukiwa cheo cha Luteni Usu.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Meja Jen. Paul Peter Massao kwa Rais Magufuli, imeeleza kuwa kati ya maafisa wote 197, maafisa 160 ni wanaume ambapo 149 ni Watanzania na 11 wanatoka nchi rafiki na maafisa 28 ni wanawake ambapo 25 ni Watanzania na 3 wanatoka nchi rafiki.

Rais Magufuli amewapongeza kwa kuhitimu mafunzo salama na kutunukiwa kamisheni na amewahakikishia askari wote wa JWTZ kuwa Serikali yake inathamini kazi zinazofanywa na Jeshi hilo na itaendeleza juhudi zilizofanywa tangu awamu zilizopita za kujenga jeshi imara, linaloheshimika na lililo tayari kutekeleza majukumu yake ya kuilinda nchi wakati wote.

Rais Magufuli pia amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kukamilisha ujenzi wa ukuta katika eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite la Mererani Mkoani Manyara, na kwa kuitikia wito wa kujenga viwanda ambapo viwanda vya Maji na nafaka vimeanza kujengwa, na pia Jeshi la Magereza kwa kuimarisha kiwanda cha kutengeneza viatu.

Katia hatua nyingine Rais Magufuli amewaapisha Majaji 2, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliowateua tarehe February 1, 2018.

Walioapishwa kuwa Majaji ni George Mcheche Masaju na Gerson John Mdemu. Rais Magufuli amemuapisha Dkt. Adelardus Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Paul Joel Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kilichozungumzwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu wake na Majaji baada ya kuapishwa na JPM

 

Soma na hizi

Tupia Comments