Mix

Ugomvi wa watoto ulianzia kwenye chakula.. mmoja wao akachukua bastola

on

BastolaUliwahi kuipata story ya mtoto kwenye AMPLIFAYA na hapa kwenye millardayo.com ambapo mtoto huyo alimshoot mama yake ambaye alikuwa mjamzito, ukiangalia movie huwa wanaweka parental guide ambayo inaelekeza kwamba mtu mwenye umri wa kuanzia miaka mingapi anaruhusiwa kuiangalia.. haya matukio ni moja ya vitu ambavyo vinazuiwa mtoto asijifunze kutoka kwenye movies hizo.

Hii ya leo inahusu tukio lililotokea huko Florida Marekani, ambapo mtoto mwenye umri wa miaka 13, amemshambulia kaka yake mwenye umri wa miaka 16 pamoja na mdogo wake mwenye umri wa miaka 6, kwa kuwapiga na risasi halafu akajipiga mwenyewe.

Polisi wamesema watoto hao walikuwa peke yao nyumbani kwao wakati mama yao akiwa kazini wakaanza kugombania chakula, mtoto huyo akachukua bastola na kuanza kuwashambulia wenzake, kaka yake alipiga simu Polisi  ambao walifika eneo la tukio na kumkimbiza Hospitali lakini mtoto aliyewapiga risasi pamoja na mdogo wake walikutwa wameshafariki.

29906170001_4135510305001_video-still-for-video-4135458285001

Polisi wakiwa eneo la tukio

Polisi wanafanya uchunguzi kujua jinsi mtoto huyo alivyoweza kupata silaha hiyo.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments