Leo January 21 2014 Mwanamitindo Mtanzania aishie na kufanya kazi New York Marekani Flaviana Matata, amekamilisha mizunguko kwenye shule alizozipa misaada na kutoa shukrani za pekee kwa waliomsaidia kwenye huu mpango wake.
Flaviana Matata Foundation Stationaries Project ni mradi ambao unajihusisha na uhamasishaji wa mashirika mbalimbali, taasisi za serikali na watu binafsi kuchangia na kusambaza vifaa mbalimbali vya shule kama madaftari, kalamu za wino, kalamu za risasi, rula, mikebe, vifutio na mabegi ya wanafunzi, kwa wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu nchini Tanzania.
Hapa ni mwanzilishi wa Flaviana Matata Foundation (FMF) ambaye ni Flaviana Matata pamoja na Afisa mawasiliano, masoko na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hawa Kikeke wakiongelea Flaviana Matata back to School.
Mradi huu unalenga kwenye elimu hasa kwa watoto wa kike lakini waliomaliza darasa la saba na kushindwa kulipa ada zao kwa ajili ya kuendelea na masomo ya sekondari kwa shule za msingi, anasema ‘tulianzisha Flaviana Matata Stationeries na kuizindua October 2013 Kwa ajili ya kutoa Stationaries Kit.
Shule ambazo mpaka sasa zimepata vifaa hivyo vya mradi huu ni pamoja na Kisarawe, Mgulani na Bagamoyo.