Habari za Mastaa

Flavian Matata afika kwa Ridhiwani na kufanya hili kwa Wanafunzi, Wazazi wafunguka

on

Mwana Mitindo mrembo Flavian Matata kupitia Foundation yake ya Flavian Matata Foundation ametoa msaada wa vifaa vya Shule kwa watoto wote wa shule ya Msinune iliyopo kata ya Kiwangwa Wilaya ya Chalinze, vifaa hivyo ni Pamoja Na Mabegi, Daftari, Kalamu, Taulo za kike za Lavy na Vifaa vya Walimu vya kufundishia

Flavian amekuwa akifanya hivi kwa Shule hii kwa miaka 6 sasa na Tayari ameshawajengea madarasa, Nyumba za Walimu, vyoo, Madawati Na vifaaa vya kufundishia

Tukio hili la leo limehudhuriwa na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambaye ameahidi kumpa ushirikiano Flavian katika kuendeleza ujenzi wa nyumba nyingine za Walimu  katika Shule hiyo.

 

RIDHIWANI AMPA FLAVIAN SHAMBA LA MANANASI, AMPONGEZA KWA KUYAFANYA HAYA KWENYE JIMBO LAKE

 

Tupia Comments