Tamasha la Coca-Cola Food Fest limefanyika jana kwa ufanisi mkubwa katika viwanja vya St. Laurent Diabetes Center, Kawe, jijini Dar es Salaam.
Tukio hili liliwaleta pamoja mastaa maarufu, waandaaji wa maudhui, na wapishi wa vyakula mbalimbali, likiwa ni sehemu ya juhudi za Kampuni ya Coca-Cola kusherehekea na kuendeleza utamaduni wa vyakula vya kiafrika na kimataifa huku kiburudisho kinachoendana na vyakula hivyo kikiwa ni soda ya Coca-Cola.
Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania, Flaviana Matata, alikuwa miongoni mwa mastaa waliohudhuria tamasha hilo. Flaviana alionyesha uwezo wake wa kipekee katika mapishi na alieleza jinsi anavyojifunza kuandaa vyakula mbalimbali kupitia mtandao wa YouTube, jambo ambalo limemuwezesha kupika vyakula vingi kwa mafanikio bila msaada wa walimu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwanamitindo huyo alisema, “Ingawa napenda sana pilau, bado nakabiliana na changamoto katika namna bora ya kuandaa pishi hili”. Pia alikumbushia kuwa chakula cha wali na maharage kina nafasi maalum maishani mwake, kwani kina mkumbusha nyakati zake za utoto.
Akihitimisha, Flaviana aliwashukuru waandaaji wa ‘Coca-Cola Food Fest’ kwa kuandaa tukio hilo, akisema liliwapa fursa mastaa mbalimbali kushirikiana, kupika, na kufurahia chakula kama marafiki katika mazingira ya kijamii yenye furaha.