Duniani

Pale ambapo mambo hayaendi sawa Rubani anaamua kutua ndege barabarani.. (Video)

on

Kuna wakati ambao ikitokea mambo yameharibika angani, Rubani wa ndege anaamua kufanya maamuzi magumu ili kuokoa abiria wake na kuhakikisha hakiharibiki kitu.

Plane

Nimekipata kipande cha video ya kama sekunde 72 hivi, jamaa walikuwa wanaendesha zao magari kwenye barabara Mitaa ya California, Marekani… wakati wamefika kwenye mataa wakasimama kusubiri kuruhusiwa kuvuka, ghafla ikakatisha ndege ndogo speed kabisa, ikaenda mbele ikasimama !!

airplane-emergency-landing.png.cf

Ripoti ya Polisi haijasema sababu ya ndege hiyo kutua kwenye barabara ya magari, ila ndani ya ndege kulikuwa na Mwalimu pamoja na Wanafunzi wanaojifunza Urubani.. wote walitoka salama na ndege ilitua salama kabisa, hakukuwa na athari yoyote iliyojitokeza japo ni mara chache sana ndege kutua mazingira kama hayo alafu isitokee tatizo.

Unaweza kuplay hizi video kuona hali ilivyokuwa mpaka ndege ikatua barabarani mtu wa nguvu.

Hiki hapa kipande kingine cha video chenye mwendelezo wa tukio hilohilo.

https://www.youtube.com/watch?v=-FNBzXwRjXE

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments