Mnamo 26 Julai, Samsung Electronics Co., Ltd. inatarajiwa kutangaza kizazi chake cha tano cha simu janja zinazokunjika (foldables): Galaxy Z Flip na Galaxy Z Fold.
Tukio hilo la uzinduzi ambapo wateja watapata nafasi ya kutazama uzinduzi wa simu hizi kote ulimwenguni, kupitia Uzinduzi mubashara linalojulikana kama #SamsungUnpacked.
Uonyeshaji wa tukio la #SamsungUnpacked utafanyika katika maduka mbalimbali ya Samsung yaliyoko Mlimani City na Palm Village yaliyoko Dar es Salaam kuanzia saa 7:00 mchana na wateja wote wanaweza kuangalia mubashara kupitia: www.samsung.com/africa_en/
Simu janja mpya za Galaxy Foldables chini ya mfululizo wa familia ya Z-series: Flip & Fold zinatarajiwa kuwa na sifa za kipekee. Fold ina kioo kikubwa na ni simu yenye uwezo inayotoa burudani ya utazamaji wa kuvutia, betri inayodumu kwa muda mrefu katika muonekano mwebamba na ikiwa nyepesi.
Galaxy Z Flip ina muundo na umbo zuri lisilo na kifani na Galaxy Z Flip inatoa uzoefu bora zaidi wa kamera kwenye simu janja za Samsung Galaxy. Mtu ataweza kupiga picha za ubora wa kiwango cha juu.
Ili kuongeza ushiriki na kupunguza mzigo wa kifedha kwa wateja, Samsung Electronics East Africa itatangaza ushirikiano na moja ya benki yenye sifa nchini Tanzania ambayo itawawezesha wamiliki wa Kadi za Visa kulipia simu zao za Z-Flip na Z-Fold na kupata discount ya punguzo la hadi asilimia 10.
Samsung imejitolea kuwapa wateja utulivu na amani kupitia Huduma ya Samsung Care+ ambayo huduma ya msaada kwa ajili ya uharibifu wa bahati mbaya wa kioo cha simu. Wateja wanaweza kusajili ndani ya siku 30 baada ya kununua Galaxy Flip na Fold na kufurahia.