AyoTV

Falz wa Nigeria amewataja wasanii wawili kutoka Tanzania kwenye collabo

on

Muziki wa kizazi kipya unaendelea kufanya vizuri kwa sasa na Tanzania imekua moja wapo ya nchi yenye wasanii wanaofanya vizuri zaidi kwenye tasnia nzima ya burudani ambapo kumekuwa na collabo nyingi za wasanii watanzania wanazofanya na wasanii wa nchi za Afrika kama Nigeria, Kenya,SouthAfrica na nyinginezo.

Millardayo.com na AyoTV  zimeweza kumpata Rapper kutoka nchini NigeriaFalz the Badh guy mmiliki wa hit single ya ‘Soldier’ na ‘Soft work’  na Goodnews ni ambapo ametaja wasanii wawili kutoka Tanzania  atakaofanya nao collabo hivi karibuni.

wasanii wa Tanzania  nnaotaka kufanya nao collabo wakwanza ni Diamond Platnumz ofcoarse, na hivi karibuni nmekutana na msanii mwingine ambae ni Joh Makini kwenye Coke studio na tumeweza kuwa marafiki wazuri sana na mtegemee collabo yangu na yeye pia‘ – Falz

ULIMISS KUITAZAMA VIDEO YA ON AIR WITH MILLARDAYO MSANII KUTOKA NIGERIA AMEMTAJA MSANII WA BONGO ANAYEMKUBALIA? UNAWEZA KUICHECK VIDEO NIMEKUWEKEA HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments