Top Stories

CHADEMA yatoa tamko Polisi kutomfikisha Lissu Mahakamani

on

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa TLS, Tundu Lissu bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni siku ya pili tangu alipokamatwa.

Ayo TV na millardayo.com ziliweka kambi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kufuatilia kama Lissu angefikishwa Mahakamani hapo lakini hadi ilipotimu saa 9:30 Alasiri ambao ni muda wa mwisho wa shughuli za Mahakama hakufikishwa.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ya CHADEMA, Tumaini Makene, amesema Chama hicho kinatarajia Lissu atapata dhamana akiwa kituo cha Kati cha Polisi.

Pia endapo kama hilo halitafanyika, wanasheria wao watachukua hatua za kisheria kuhusiana na hilo.

Tundu Lissu alikamatwa August 22, 2017 wakati anatoka katika Mahakama ya Kisutu ambapo alikuwa anafanya kazi zake za uwakili katika kesi ya makosa ya kimtandao inayomkabili Yericko Nyerere.

BAVICHA wazungumza ishu ya Lissu kuwekwa ndani na mengine…tazama hapa!!

Soma na hizi

Tupia Comments