Mali za Mastaa

Listi ya wanamichezo matajiri imetoka! Ronaldo, Mayweather, Pacquiao, Messi, nani amekamata namba 1?

on

  Jarida namba moja kwa masuala ya fedha, Forbes kutoka nchini Marekani limetoa listi ya wanamichezo walioingiza fedha nyingi zaidi duniani katika kipindi cha miezi 12 iliyopita…

Floyd Mayweather

 1. Floyd Mayweather Jr.

Mapato yote: Dola Mil. 300

Malipo ya Mapambano ya Ngumi: Dola Mil. 285

Dili za Matangazo ya Biashara: Dola Mil. 15

Mapato ya Dola Milioni 300 kwa mwaka yanavunja rekodi mapato makubwa zaidi aliyowahi kuingiza mwanamichezo yoyote kwa kipindi cha mwaka 1. Rekodi iliyopita ilikuwa ikishikiliwa na Tiger Woods aliyeingiza Dola Milioni 115 mwaka 2008.

Emmanuel “Manny” Dapidran Pacquiao

 2. Manny Pacquiao
Mapato ya Jumla: Dola Milioni 160

Mshahara: Dola Milioni 148
Matangazo ya Biashara: Dola Milioni 12

Fedha aliyolipwa Pacquiao Dola Milioni 125 kwenye pambano lake na Mayweather ilikuwa mara nne zaidi ya fedha aliyopata katika pambano lake lilopita alipopigana na Chris Algieri. Mapato mengine yametokana na dili za Mikataba yake na Kampuni za Nike, Foot Locker, Wonderful Pistachios, na matangazo mengine.

Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro

 3. Cristiano Ronaldo

Mapato ya Jumla: Dola Milioni 79.6

Mshahara/Posho/Bonus: Dola Milioni 52.6
Matangazo ya Biashara: Dola Milioni 27

Akiwa bado anashikilia tuzo ya mwanasoka bora wa dunia, Ronaldo ndio mwanasoka anayelipwa fedha nyingi duniani huku akiwa amemzidi hatua moja mbele mpinzani wake Lionel Messi.

Lionel Andrés “Leo” Messi Cuccittini

4. Lionel Messi

Mapato ya Jumla: Dola Milioni 73.8

Mshahara/Posho/Bonus: Dola Milioni 51.8
Dili za Matangazo ya Biashara: Dola Milioni 22

Roger Federer

  1. Roger Federer

Mapato ya Jumla: Dola Milioni 67

Mshahara: Dola Milioni 9
Dili za Matangazo: Dola Milioni 58
Pamoja na kutokuwa na mafanikio makubwa uwanjani, lakini Federer tayari ni bingwa wa mara 17 wa mataji makubwa ya tennis na anaingiza fedha nyingi kutokana na mikataba yake ya kibiashara kama Nike, Rolex na Credit Suisse.

Mwaka 2014 aliongeza mkataba wake na Mercedes Benz kwa miaka 3.

Tupia Comments