Top Stories

UPDATES: Tundu Lissu kahojiwa kwa tuhuma za makosa mawili

on

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye alikamatwa na Polisi mapema leo wakati anatoka Mahakamani, amehojiwa na Polisi kwa tuhuma za kufanya makosa mawili.

Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene amesema, Tundu Lissu alihojiwa na Polisi kuhusiana na makosa mawili ambayo ni;

1. Kumkashifu Rais.

2. Uchochezi kuhusu kuzuiliwa na kushikiliwa kwa Ndege ya Serikali ya Bombardier.

Tundu Lissu anadaiwa kufanya makosa hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ijumaa iliyopita, August 18, 2017.

Aidha, Makene amesema, Lissu ambaye ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amekataa kutoa maelezo yoyote Polisi, akitumia haki yake ya kisheria kuwa mtuhumiwa ana haki, kisheria, kutaja jina na anuani yake tu anapokuwa anashikiliwa na Polisi hadi atakapofikishwa Mahakamani ambako ndiko atataoa maelezo kujibu mashtaka anayotuhumiwa nayo.

Lissu amesema yuko tayari kujibu mashtaka yake Mahakamani ambapo akiwa Polisi amepata msaada wa kisheria kutoka kwa Wakili Faraji Mangula, ambaye pia anashughulikia uwezekano wa mteja wake kupata dhamana kwa mujibu wa sheria.

Soma na hizi

Tupia Comments