Top Stories

IGP Sirro kalipangua tena Jeshi la Polisi

on

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro leo August 24, 2017 amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Juma Yusuf Ally kuwa Kaimu Kamishna wa Polisi Zanzibar ambapo atachukua nafasi ya aliyekuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdani Omari Makame alieystaafu kwa mujibu wa sheria baada ya kutimiza umri wa miaka 60.

Kabla ya uteuzi huo DCP Juma alikuwa Mkuu wa Utawala na Fedha Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.

Aidha, IGP Sirro amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lazaro Mambosasa kuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambapo kabla ya uteuzi huo, SACP Mambosasa alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Neema Mwalimu Mwanga anakwenda Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.

IGP Sirro pia amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Gilles Bilabaye Mroto kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Emmanuel Lukula kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke.

Kabla ya uteuzi huo, ACP Lukula alikuwa Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Mbeya.

ULIPITWA? MWANZO-MWISHO: IGP Sirro aenda Kibiti na Mkuranga…tazama hapa chini kwenye hii video!

Soma na hizi

Tupia Comments