Habari za Mastaa

PICHA 20: Kim Kardashian aweka hadharani picha za ndoa yake na Kanye West

on

Mrembo Kim Kardashian ameamua kuziweka hadharani picha za harusi yake na mume wake Kanye West ambazo hazikuwahi kuonekana, harusi hiyo ilifanyika May 2014 nchini Italia na ilikuwa miongoni mwa harusi ambayo ilichukua headlines kwenye mitandao ya kijamii.

Harusi hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali maarufu akiwemo mwanamuziki John Legend na mkewe Chrissy Teigen na muongozaji wa filamu ya 12 Years a Slave Steve McQueen na wengine kibao,ilielezwa kuwa kampuni ya Adidas ilichagua siku hiyo ya harusi kuzindua tangazo lao la kombe la dunia kwa mwaka 2014 lililomhusisha rapa Kanye West pamoja na mastaa wakubwa wa soka duniani Lionel Messi na Dani Alves.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Kim Kardashian aliandika “Miaka mitano nyuma niliolewa na rafiki yangu wa karibu, nyuma ya pazia kilichotokea miaka mitano nyuma kwenye harusi yetu”

VIDEO: SANCH AZUNGUMZA PICHA ZAKE ZA NUSU UTUPU, JE ANAJIUZA?, ISHU YA DAVIDO NA DON JAZZ

Soma na hizi

Tupia Comments