Michezo

Makambo kaondoka Yanga SC?

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga SC raia wa Congo DR Heritier Makambo ametangazwa kuwa amesaini mkataba na club ya AC Horoya ya Guinea taarifa ambazo bado hazijathibitishwa kwa upande wa Yanga wala kutolewa taarifa zozote.

Kinachomsambaa katika mitandao ya kijamii ni Makambo akiwa kaonekana na jezi ya AC Horoya ya nchini Guinea, picha ambayo inaashiria kuwa staa huyo kaamua kutimka Tanzania na kwenda kuendeleza maisha yake nchini Guinea.

Makambo aliyewahi kucheza club ya FC Lupopo ya kwao Congo, amehusishwa kuwa ameuzwa na Yanga huku baadhi ya watu wanahoji kimya cha Yanga katika dili hilo, wanasema hawakupanga kumuuza ila staa huyo ameamua kuondoka baada ya kumaliza mkataba na kutotaka kuendelea kutokana na mazingira ya kazi Yanga yalivyo kwa sasa, taarifa bado hazijathibitika wanasubiriwa Yanga.

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments