Habari za Mastaa

Yakufahamu baada ya Alikiba kuandikwa kwenye Jarida la Marekani……

on

Kama utakuwa unakumbuka kati ya mambo 7 yatakayoanza kujitokeza baada ya Alikiba kusainiwa Sony Music ni hili la kuandikwa kwenye jarida la Marekani linaloandika habari za mastaa wa muziki ‘The Source Magazine’.

Meneja wake aitwae Seven aliwahi kuiambia millardayo.com na kusema >>>Alikiba anakuwa msanii wa kwanza wa Tanzania kusaini mkataba na Sony World wide, ni mkataba wa miaka mitano, habari yake sio ndogo na sasa atatokea ameandikwa na Jarida maarufu la habari za mastaa Marekani The Source Magazine’

DE445555

Sasa leo August 9, 2016 staa huyo aliwataarifu mashabiki wake kupitia instagram baada ya kuandikwa kwenye jarida hilo na kuyaandika haya>>>The 1st Bongo Flava artist in history to be featured in the THE SOURCE MAGAZINE! I’m proud to place BongoFlava on cover feature of the number #1 MusicMag on the Planet! Show love to The Source’

‘Atakua msanii wa kwanza wa Afrika Mashariki kuandikwa ndani ya hili jarida na hii itamsaidia kujulikana zaidi sababu ni jarida linaloaminika na linalosomwa na mamilioni ambapo kichwa cha habari kitasomeka kuanzia ukurasa wa mbele wa jarida hili’ – Seven

ULIKOSA KUONA ALIKIBA ALIVYOSAINI NA SONY SOUTH AFRICA? HAYA NI MAMBO MANNE KATI YA YOTE ATAYOYAPATA KWENYE MKATABA WAKE MPYA.

Soma na hizi

Tupia Comments