Habari za Mastaa

Models wengi ni wembamba, Ufaransa unadhani wanawataka hao??

on

f_6cbc2c3fbb5e8ecc927db404726d43efthe-fashion-industryKama ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya urembo utagundua kuwa wasichana wengi wanofanya maonesho ya mitindo ya mavazi na masuala la urembo wana maumbo madogo madogo hivi.. wengi ni wembamba, hivi umewahi kuona eti mwanamitindo mnene hivi?

Bunge la Ufaransa limepitisha Sheria inayopiga marufuku makampuni yanayojihusisha na masuala ya mitindo nchini humo kutumia wasichana wembamba kupita kiasi.

05fashionWatu wanaofanya kazi ya kuwatumia models wanatakiwa kuanzia sasa watumie wasichana au wanawake ambao sio wembamba sana, ila wawe na wembamba ambao ni salama kiafya, yoyote akienda kinyume ni faini ya Euro 75,000 hivi ambazo Bongo ni zaidi ya Mil. 140 pamoja na Mmiliki wa Kampuni inayohusika kufungiwa kwa zaidi ya miezi sita.

Usishtuke na hii mtu wangu, nimepita mitandaoni na kuona kumbe Israel iliweka Sheria hiyo pia mwaka 2013, Italy na Spain wao walitengeneza kanuni ambazo zinasaidia pia kuzuia kutumia wanawake wembamba sana na waliodhoofu.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments