Michezo

Fahamu alichosema kocha wa zamani wa FC Barcelona kuhusu kufundisha

on

Barcelona coach Frank Rijkaard (L) and tKocha wa zamani wa timu ya Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi Frank Rijkaard amechukua uamuzi ambao umewashtua watu wengi wapenda soka duniani.

“Kwa namna mambo yalivyo sasa natangaza sitokuwa kocha mkuu tena. Sina matamanio ya kurudi kufundisha tena,’ aliliambia jarida la  Voetbal International katika mahojiano yaliyochapishwa Jumatano.

Kocha huyo mwenye miaka 51 amekuwa nje ya soka kwa takribani miezi 14 baada ya kufukuzwa kuwa kocha wa Saudi Arabia mwezi January mwaka jana.

“Nina shukuru kwa kila kitu nilichofanikiwa kwenye soka lakini sasa ningependa kufanya vitu vingine, kutoka kwenda kuangalia soka na kujadili mechi hizo baada ya hapo. Sina matamanio ya kuwa mzee wa miaka 60 ambaye bado anaendelea kuwa uwanjani kufundisha soka,” alisema Rijkaard.

 

Tupia Comments