AyoTV

Utaratibu umetangazwa game ya Mabingwa wa zamani wa Europa League vs Simba SC

on

Kuelekea mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Simba SC dhidi ya Mabingwa wa Europa League mara tatu mfululizo club ya Sevilla ya nchini Hispania, imetangazwa kiingilio vya mechi hiyo ambayo itachezwa Dar es Salaam Tanzania siku ya May 23 2019 saa 19:00 EAT kwa ajili ya kuvutia watu wengi.

Game hiyo pamoja ya kuwa ya viwango vya juu na kimataifa itachezwa saa 19:00 EAT kutokana na watu wengi kuwa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, hivyo wameweka muda huo ili kuepuka kuingiliana na muda wa waumini wa dini ya kiislanu wa kufuturu.

Tiketi za kuingia katika mchezo huo ni gharama nafuu pamoja na kuwa zinahusisha timu yenye ushindani mkubwa nchini Hispania, VIP B ni Tsh 15,000 wakati kiingilio cha gharama za chini zaidi kitakuwa ni Tsh 5000 kwa mzunguuko huku ikielezwa kuwa kutakuwa na huduma ya tiketi za VIP Platnumz watakaopatiwa huduma maalum.

Samatta kaweka historia Ubelgiji, mchezaji wa tatu kuwahi kushinda Ebony Award 2019

Soma na hizi

Tupia Comments