Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imewahukumu Fred Nyagawa, Isaya Mgimba na James Mteleke kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua kwa kukusudia Mchape Mkosa, hukumu hiyo imetolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe katika shauri la jinai No. 34/2017.
Mahakama imesema mauaji hayo yalifanyika mnamo December 17, 2015 katika kijiji cha Mapogolo kilichopo Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe.
Mahakama imesema aliyeuawa (Mchape) alikuwa ni Dereva Bodaboda ambaye siku ya tukio alikodiwa na walipofika maeneo ya kijiji cha Mapogolo alinyang’anywa pikipiki na kuuawa kisha Wauaji kutoweka na pikipiki hiyo kwenda kuiuza mkoani Mbeya ambako baadaye ilikamatwa.
Mahakama imesema ilidaiwa kuwa chanzo cha mauaji hayo ni tuhuma za ugomvi wa mashamba na uchawi kwamba Mchape alikuwa akiwaroga Familia ya Mshtakiwa wa kwanza na wa nne ambao ndio waliwatafuta Washtakiwa wengine wa pili na watatu ili kumuua Mchape kwa malipo ya Tshs. 2,000,000 na walilipwa fedha hizo baada ya kutekeleza mauaji hayo.
MZEE ANAISHI NA MAMBA TANZANIA, ANAONGEA NAE KAMA MTOTO WAKE, ANAMUITA “AJABU”