Top Stories

Fred Lowassa afanya ziara Monduli, achangia zaidi ya Milioni 6 (+picha)

on

Mbunge wa Jimbo Monduli , Fredrick Lowassa amefanya ziara jimboni kwake ambapo ametembelea eneo litakalojengwa nyumba ya Daktari , eneo la Shule ya Msingi ya Indonyonado iliyoezuliwa na upepo, pamoja na Zahanati ya Kata iliyopo Engutoto Kijiji cha Mlimani.

Katika ziara hiyo waliyofanya Aprili 2, 2021 aliambata na Mkuruagenzi wa ECLACT Foundation ,Peter Toima nakuchangia zaidi ya Shilingi 11 milioni za mfuko wa jimbo lake.

Aidha baada ya kufanya ukaguzi wa maeneo hayo Lowassa ambaye kipaumbele chake ni “elimu” alizungumza na wananchi nakuwashukuru kwa kumchagua kwa kura nyingi kwa asilimia 93.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la ECLAT DC, Peter Toima alimshukuru Lowassa kwa kumkaribisha jimboni kwake na kuahidi kumuunga mkono kwa dhati ambapo alitoa Sh 5milioni kuweka katika mfuko wa jimbo.

MEI MOSI: “TULIKUJA NA MATARAJIO YAKUONGEZWA, HATA KWA PUNGUZO TUNASHUKURU”

Soma na hizi

Tupia Comments