Mbunge wa jimbo la Monduli Fredy Lowassa amesema ili kuendana kasi ya mabadiliko ya teknolojia duniani na mabadiliko ya tabia nchi jamii za kifugaji hazina budi kuwekeza katika elimu kwa watoto wao.
Fredy amesema kwa hali ilivyo sasa ni lazima jamii ya wafugaji kubadilika na kijikita kuekeza katika elimu na kuachana na dhana ya kuwa na idadi kubwa ya mifugo kutokana na changamoto ya ardhi ambayo haiongezeki lakini idadi ya watu ikiongezeka.
Fredy ametoa wito huo wilayani Monduli mkoani Arusha wakati akikabidhi vifaa mbalimbali kwa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 katika shule mbalimbali wilayani humo kama jitihada mbunge huyo kuahakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanajiunga na elimu ya sekondari.
Aidha Freddy amewataka wananchi wa Monduli kuenzi mawazo ya waziri mkuu msataafu Edwad Lowasa ambae ni mwasisi wa shule za kata kwa kuwatendea haki watoto wa jamii ya kimaasai kwenda shule.