Baada ya Future na Drake kufanya kazi kwa pamoja na kuachia mixtape iliyopewa jina ‘What A Time To Be Alive’, wasanii wengine wa Hip Hop wameona sio mbaya wakifuata ramani ya Future na Drake.
Rapper French Montana na Fetty Wap wamekuwa wakishirikiana kwenye nyimbo nyingi kipindi hiki na kwa mujibu wa kaka yake French Montana na mkurugenzi wa lebo ya Coke Boys Music, Zack.. taarifa ikufikie kwamba wawili hao wapo studio kutengeneza mixtape yao mpya iliyopewa jina ‘Coke Zoo’.
>>> “Kwa sasa mixtape hiyo itakuwa na nyimbo saba, moja nikiwa nimeshirikishwa pia, na baadhi ya single zimewekwa online pia…” <<< alisema Zack Mkurugenzi wa Coke Boys Music.
Wakati tukiwa tunaendelea kusibiri ujio wa mixtape hiyo kutoka kwa French Montana na Fetty Wap, nimeona itakuwa poa kama nikishare na wewe single yao iliyotoka hivi kariuni ‘Freaky’… Kama ilikupita na mpaka sasa hujaisikia basi karibu ukisikilize hapa chini mtu wangu.
https://youtu.be/XXknLYBVG_c
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.