Bomoabomoa ilianza mwishoni mwa mwaka 2015 kwenye baadhi ya maeneo Dar es salaam hasa ya mabondeni na maeneo ya kando na mto Msimbazi ambapo zoezi hilo lilisitishwa baada ya kesi kufunguliwa kupinga ubomoaji wa nyumba 2619 za wakazi wa Tabata Segerea mwigizaji Wastara akiwa miongoni mwao.
Wastara amekaa kwenye Exclusive Interview na millardayo.com na AyoTV leo na kusema yafuatayo >>> ‘Baada ya kuona kuna bomoabomoa inakuja nikahangaika nikapata pesa ya kununua nyumba sehemu nyingine ili nipate pa kuwahifadhi watoto wangu na watoto yatima ninaowalea na kuishi nao’
‘Nimehangaika kwa nguvu zangu kwa hela halali bila kupewa na mtu nikapata hiyo nyumba nyingine, nashukuru pia baada ya kufikiria kupata nyumba mpya huku kwenye nyumba zilizopigwa X tukapewa ruhusa ya kuendelea kukaa na kutafuta leseni za makazi‘ – Wastara
ULIIKOSA HII YA WASTARA KUELEZEA KWANINI NDOA YAKE NA MBUNGE IMEVUNJIKA NDANI YA SIKU 80.