Mix

PICHA 4: Msafara wa Makamu wa Rais Samia Suluhu wapata ajali Mtwara

on

Ni September 9, 2016 ambapo Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia suluhu hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya mtwara,majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka mtwara kuelekea tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.

.

.

.

.

.

.

.

.

Endelea kukaa karibu na millardayo.com & Ayo TV tunaendelea kukuhabarisha zaidi taarifa zinapotufikia

ULIKOSA ALICHOKIZUNGUMZA RAIS MAGUFULI BAADA YA KUWATEMBELEA WAKAZI WA MAGOMENI KOTA BASI BONYEZA PLAY HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments