AyoTV

Patoranking kajibu kwanini hakuna msanii wa Afrika Mashariki kwenye album yake

on

Ngoma yake ambayo ilikua kubwa sana Tanzania na Afrika kwa ujumla ni ‘my woman‘ ambapo sasa staa huyu wa Nigeria aitwae Patoranking amekuja Dar es salaam Tanzania kufanya Interview na media kuipromote album yake mpya.

AyoTV na millardayo.com zimempata kwenye Exclusive na kusema kwanini kwenye album nzima ya God Over Everthing hakuna msanii hata mmoja wa Afrika Mashariki aliyemshirikisha.

‘Ni album ambayo nimewashirikisha watu kama Wizkid, Olamide na wengine kutoka Nigeria, sijawashirikisha wa Afrika Mashariki na pande nyingine sababu ni album yangu ya kwanza, nilitaka iwe album ambayo nitatangaza Nigeria kwanza lakini album ijayo nitawashirikisha wa Afrika Mashariki na wengine hakuna neno’ – Patoranking

ULIIKOSA HII KAULI YA KWANZA YA JACKLINE WOLPER BAADA YA KUJIUNGA CCM AKITOKEA UKAWA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments