Habari za Mastaa

Mengine mapya kutoka msikitini kuhusu Mzee Yusuf kustaafu muziki

on

Ni August 12, 2016 ambapo nguli wa muziki wa Taarab mzee Yusufu amechukua headlines katika vyombo mbalimbali hasa mitandaoni kuhusiana na kutangaza kuacha kazi ya muziki wa Taarab na kuaamua  kuishika zaidi dini yake ya Kiislamu hivyo hatofanya tena muziki wa Taarabu.

Sasa leo August 16 tumempata imamu wa msikiti wa Ilala Bungoni (Masjdi Taqwa) Mohamed Issa na kuyaongea haya>>>>Suala hili tuliambiwa na shekh yetu siku ya Alhamisi kwamba Ijumaa Shekh  Yusuf atakuja kusali hapa na kutangaza rasmi kuacha muziki wa Taarab na mungu akamjaalia IJumaa akaja na kusaliwa sala ya Ijumaa huku akapewa muda wa kuzungumza lakini macho yanamtoka’- 

Aliwaomba wadau na wapenzi wa muziki wake kuacha kutumia kazi zake kutokana na yeye kuingia kwenye masuala ya dini, kwahiyo mimi kama imamu naomba Mungu amjalie kwa vitu anavyotaka baada ya kuingia kwenye kumsalia Mungu’- 

Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Imamu Issa Mohammed kuhusu Mzee Yusuf

ULIIKOSA HII YA MC PILIPILI KWENYE HARUSI YA MCHEKESHAJI MASANJA BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments