Habari za Mastaa

Dude kuileta Bongo Dar es Salaam October 2016?

on

NI Sept 20, 2016 ambapo msanii kutoka Bongo Movie, Dude amefunguka kuhusu maandalizi ya kuirudisha kipindi cha Bongo Dar es Salaam katika luninga.

Akiongea na millardayo.com & Ayo TV staa huyo alisema…>>>Kwanza nilikuwa najaribu kufanya mazungumzo na wamiliki wa vituo vya luninga ili niweze kurusha kipindi changu cha Bongo Dar es Salaam na sio kama nahitaji pesa nyingi sana lakini nahitaji aghalau nirudishe maandalizi ya kazi yangu’

‘Takribani tukiacha mwezi huu wa tisa upite tutegemee mwezi wa kumi nadhani kila kitu kitakuwa vizuri na nitaweza kutengeneza vipindi vingi zaidi na mwezi wa kumi nina uhakika kabisa kuwa kipindi kitakuwa hewani lakini sitotaka kuwaambia mashabiki zangu kuwa ni TV gani kitakuwa kinarusha ila wakae mkao wa kula’

Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Dude kuhusu Bongo Dar es Salaam

ULIIKOSA HII YA WEMA AKICHEZA VIGOMA KWA WATU WAKE WA MKOANI TANGA BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments