Habari za Mastaa

Nay wa Mitego ndio kamalizana na BASATA? sikia alichosema

on

July 16, 2016 Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) lilitoa tamko la kuufungia wimbo wa msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego uitwao ‘pale kati‘ kwa kigezo cha kutokuwa wa madili lakini pia BASATA walitangaza kumfungia Nay kutoshiriki kazi yoyote ya kisanii.

Sasa Agosti 2, 2016 staa huyo amepatikana kwenye Exclusive ya millardayo.com na AyoTV kayaongea haya >>> ‘Mimi na basata tumeshamalizana kuanzia sasa hivi watu waendee tu ku-request wimbo unaendelea kupigwa media zote mimi na basata tumeyamaliza, wimbo una version mbili na video nne tofauti’

Video ya kwanza itaanza kutoka wiki ijayo, version ya pili ya audio ya ‘pale kati’ ndio ina marekebisho ambayo yalifanywa kutokana na maagizo ya BASATA, wimbo huu hautakuwa na utofauti sana na ule wa mwanzo ila maneno machache tu nimebadili kama walivyotaka‘ – Nay

Je Nay atajibu nini kuhusu ishu ya yeye kuzuiwa kufanya kazi za kisanii na BASATA? bonyeza play hapa chini

ULIIKOSA HII YA BASATA KUHUSU KUMFUNGIA NAY WA MITEGO KUTOFANYA BONGO FLEVA BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments