Alhamisi ya July 13 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam iliandikwa historia mpya kwa club ya Everton ya England kucheza kwa mara ya kwanza katika historia ya club hiyo katika ardhi ya Tanzania wakicheza dhidi ya Bingwa wa SportPesa Super Cup Gor Mahia ya Kenya.
Everton ambao wameanza maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England wakiwa na staa wa zamani wa Man United Wayne Rooney, wameanza kwa ushindi wa magoli 2-1, magoli ambayo yalifungwa na Wayne Rooney aliyepiga shuti la mbali dakika ya 34 na dakika 3 baadae Gor Mahia wakasawazisha.
Kocha wa Everton ambaye mchezo huu ameutumia kama kupima wachezaji wake uwezo, alibadilisha kikosi chake chote kipindi cha pili ndipo kipindi cha pili Dowell dakika ya 77 akapachika goli la pili na kuufanya mchezo kumalizika kwa magoli 2-1.
Goli pekee la Gor Mahia lilifungwa na Tuyisenga dakika ya 37 ya mchezo ikiwa ni dakika 3 zimepita toka Wayne Rooney afunge goli la kwanza la Everton, baada ya mchezo huo Everton watacheza mchezo wao wa pili wa maandalizi ya msimu dhidi ya FC Twente ya Uholanzi July 19.
VIDEO: Ulinzi aliyoingia nao Wayne Rooney uwanja wa Taifa leo