Mix

Taarifa kuhusu ajali ya moto ulioteketeza shule ya msingi.

on

fire-and-explosion-accidents

Hii sio picha halisi ya ajali ya moto huo.

Moto mkubwa umeteketeza majengo ya Shule ya msingi Filbert Bayi na kisha kusambaa na kuteketeza mabweni yote ya Wanafunzi pamoja na madarasa.

Mwenyekiti wa shule hiyo Filbert Bayi amesema moto huo ulianza saa nane usiku katika bweni la wanafunzi wa kike na kisha kusambaa shule nzima kutokana na gari za zimamoto kuchelewa kufika mapema.

20141111_130601

Hakuna mwanafunzi yoyote aliyejeruhiwa wala kudhurika kutokana na moto huo.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani kamishna mwandamizi wa Polisi Litrichi Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa taarifa kamili juu ya chanzo cha moto huo zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.

Bonyeza play kusikiliza taarifa iliyoripotiwa na televisheni ya TBC 1 kuhusu ajali hiyo.

Kama utapenda kutopitwa na kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments