Michezo

Full Time za Barcelona vs PSG na Bayern vs Porto ninazo hapa.

on

Hatua ya 8 bora ya michuano ya klabu ya bingwa Ulaya imeendelea tena usiku wa April 21 2015 katika raundi ya pili ya hatua hiyo ambapo Barceleona waliikaribisha PSG Camp Nou na FC Bayern nao walikuwa na mzigo wa kugeuza matokeo ya wiki iliyopita mbele ya FC Porto.

FC Barcelona wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani leo wamefanikiwa kuvuka kwenda hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga PSG kwa magoli 2-0 na hivyo kupata ushindi wa jumla wa 5-1 ambapo Neymar alifunga magoli yote mawili katika mchezo huo.

Huko nchini Ujerumani katika uwanja wa Allianz Arena, FC Bayern wamefanikiwa kuiondoa FC Porto kwenye michuano hii kwa ushindi wa 6-1.

Magoli ya Bayern yalifungwa na Alcantara, Boeteng, Lewandoski aliyefunga mawili, Muller na Xabi Alonso akifunga la 6 huku Jackson Martinez akifunga goli moja la Porto ambapo kwa ushindi huo Bayern anaing’oa nusu fainali akiwa na jumla ya ushindi wa magoli 8-4.

Ligi hii itaendelea kesho kwa mechi ya Atletico Madrid vs Real Madrid na mechi nyingine ni Juventus vs Monaco.

Tupia Comments